Write your own article idiot!
error: Content is protected !!

Tuesday, June 5, 2018

KISWAHILI: FORM TWO: Topic 1 - UUNDAJI WA MANENO

 Join Our Groups

TELEGRAM | WHATSAPP


Schemes of Work 2024


English Course - Free


Kenya Resources






TOPIC 1: UUNDAJI WA MANENO

Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.

KUTUMIA UAMBISHAJI 

Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.

Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.
Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.

Mfano 1
Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.

Angalia mifano ifuatayo:

Neno
Viambisha Awali
         Kiini Viambisha
Tamati
Unapendelea
       u-na-                      
               -penda         
el-e-a
Waliongozana
       wa-li-
               -ongoz-
an-a
Analima
        a-na-
                 -lim-
  -a
anayeiimbisha
       a-na-ye
                 -imb-
-ish-a

Dhima za Mofimu



Baadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:

1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule. MfanoFundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.

2. Uambishaji huonyesha nafsi

3. Uambashaji huonyesha njeo (muda)

4. Uambishaji huonyesha urejeshi

7. Uambishaji huonyesha ukanushi

8. Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi

Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.

Vitenzi
  Kiini
  Nomino
 Vitenzi
Cheza
  -chez-
  Mchezaji, mchezo
  wanacheza/atamchezea
Piga
  -pig-
  Mpigaji, Mpiganaji
  watanipiga, aliyempiga/wanaompiga


Uambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.

Neno (Kiwakilishi)
 Kiini
   Kielezi
Huyu, Huyo
  Hu
    Humu, humo
Wangu, wako,wake  
  wa
Hii, hizo, hiki
   hi

Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.

Mfano: Hawakulima
1. Ha-, kiambishi cha ukanushi
2. Ku-, kiambishi njeo/wakati

Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.
Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.

Mfano

Neno
   Viambishi Tamati
Anapiga
              -a
Wanapigana
             -an
Asipigwe
              -w
Amempigisha
              -ish-

Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.

Neno
    Kiini
Viambishi Tamati
Piga
      pig-
              -o
Mchezo
     chez-
              -o
Mtembezi
     tembe-
              -z-i
Mfiwa
      -fi-
              -us-a


KUTUMIA MNYUMBULIKO

Mnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu wa kitu hicho.

Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.

Viambishi vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-w-a.

Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina, kwa mfano:

Neno
Kiini
  Shina
      Maneno ya Mnyumbuliko
Elekea
 elek
   eleka
      Elekeana, elekea, elekwa, elekesha
Shikishana
 shik
   shikisha
      Shikishana, shikisha, shikishaneni

Kwa ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi mmoja wa maana.

Dhima ya Uambishaji na Mnyambulikoa wa Maneno

Dhima ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na wingi katika ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno.

Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia Mnyambuliko

Uundaji wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya matendo pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.

Zoezi 1
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko

Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbali

Maneno ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda, kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka, kauli ya kutendesha, kauli ya kutendana, na kauli ya kutendama.

Zoezi 2
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbal






EmoticonEmoticon