Write your own article idiot!
error: Content is protected !!

Saturday, June 23, 2018

KISWAHILI: FORM THREE: Topic 3 - MAENDELEO YA KISWAHILI

 Join Our Groups

TELEGRAM | WHATSAPP


Schemes of Work 2024


Necta Timetables 2024


English Course - Free


Kenya Notes






TOPIC 3: MAENDELEO YA KISWAHILI

ASILI YA KISWAHILI

Neno asili ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Kutokana na fasili hii tunaona kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa.

Hivyo basi asili ya lugha ya Kiswahili bado ni mjadala mrefu ambapo wataalamu mbalimbali wanahitilafiana juu ya asili au chimbuko la lugha ya kiswahili. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati na dini ya kiislamu. Wengine wanashikilia msimamo kuwa kiswahili ni kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na uchotara baadhi yao wanaoshikilia msimamo huu ni Freeman Grenville na Homo Sasson

Kuna nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea asili ya Kiswahili, miongoni mwa hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:


Kiswahili ni Kiarabu

Hapa Kiswahili kimefasiliwa kuwa asili yake ni kiarabu, wanaoshikilia mtazamo huu wanahoji kwamba katika lugha ya Kiswahili kuna maneno mengi ya Kiarabu. Pia wanaeleza kuwa asili ya Kiswahili ni pwani na kwa kuwa wenyeji wa pwani ni Waislamu na kwa kuwa uislamu uliletwa na Waarabu basi hii lugha ya pwani nayo itakuwa imeletwa na Waarabu. Vigezo hivyo vyote vina udhaifu mkubwa kwa sababu havikukitwa katika misingi ya kitaalamu ya uainishaji lugha.


Kiswahili ni Lugha Chotara

Mtazamo huu umezua ubishi mkubwa kwani hata baadhi ya wazawa wamejinasibisha na uarabu na ushirazi. Wanaofasili Kiswahili kama lugha chotara wanadai kuwa Kiswahili kimetokana na mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za Kibantu. Hivyo Waswahili ni watu waliotokana na wanaume wa Kiarabu na wanawake wa Kibantu.


Kiswahili ni Lugha ya Vizalia

Waumini wa mtazamo huu wanadai kuwa Kiswahili kilianza kama pijini ya Kiarabu na baadae kukomaa na kuwa kreoli. Pijini ni lugha ambayo imetokana na mchanganyiko wa lugha mbili tofauti yaani Kiarabu na lugha za Kibantu. Na kreoli ni lugha inayozungumzwa na watoto waliozaliwa na baba Mwarabu na mama Mbantu.


Kiswahili ni Kikongo

Nadharia hii inafafanua kuwa lugha ya Kiswahili ilianzia huko Kongo na kusambaa katika pwani ya Afika Mashariki. Wabatu walipofika Afrika Mashariki waliingia kwa makundi na katika nyakati mbalibali. Makundi hayo yalianza kujigawa na kutawanyika, matokeo ya kugawanyika huko ni kutokea kwa makundi mbalimbali ya wabantu. Inasadikika kuwa baadhi ya Wabantu walifanya maskani yao ya kudumu katika mabonde ya kaskazini mwa mto tana. Kikundi hiki cha wabantu ndicho inasadikiwa kuwa chimbuko la Kiswahili


Kiswahili ni Kibantu

Mtazamo huu ni ule unaoamini kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu ambapo lugha za Kibantu zilikuwepo hata kabla ya majilio ya wageni kutoka Ajemi, Arabuni, India, China na kwingineko. Katika mtazamo huu lugha ya Kiswahili inaingizwa katika kundi la lugha za Kibantu. Ama kwa hakika mtazamo huu ulipata mashiko sana kuanzia karne ya ishirini, ulishadidiwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na weledi wa isimu, historia, akiolojia na ethnografia. Wanaisimu waliothibitisha kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu ni pamoja na Bleek (1862), Meinholf. C (1932), Malcom Guthrie (1967, 1970, 1971), Doke (1935, 1945) na wengineo. Vigezo vilivyotumika kufafanua kuwa Kiswahili ni kibantu ni pamoja na:   
- Msamiati    
- Mofolojia     
- Mfumo wa sauti     
- Mfumo wa toni      
- Mfumo wa ngeli          
- Mpangilio wa maneno


Ubantu wa Kiswahili: Kigezo cha Kiisimu

Kigezo hiki cha kiisimu kimetumiwa na wataalam mbalimbali katika kuonesha ubantu wa Kiswahili Massamba (1999) amewataja wataalam mbalimbali ambao wamehusika na utafiti juu ya ubantu wa Kiswahili, wataalam hao ni pamoja na Carl Meinhof katika kitabu chake chaIntroduction to the phonology of the Bantu language,Duke (1935 – 1945), Malcom Guthrie (1967), Dereck Nurse na Thomas Spear (1985). Hawa walijadili ubantu wa Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kiisimu, kihistoria na kiakiolojia.

Katikakigezo cha kiisimu vipengele vinavyoangaliwa ni kama vile kufanana kwa msamiati wa msingi, muundo wa kifonolojia, muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia mpangilio wa ngeli za majina.

Mizizi ya msamiati wa msingi wa lugha za kibantu na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa, mifano ifuatayo huweza kuonesha ukweli huu.

Mfano
Kiswahili
             Kikurya
             Kinyiha
           Kijita
Maji
             Amanche
             Aminzi
           Amanji
Jicho
             Iriso
             Iryinso
           Eliso

Katika mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa mizizi maji, manche, minzi, manji inafanana kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo huu ni ushahidi tosha kutuonesha kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.

Pia mofolojia ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa kiasi kikubwa, yaani mfumo wa maumbo ya maneno ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibatu hufanana. Kwa mfano, namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno hufuata kanuni ileile kama inavyotumika katika lugha ya Kiswahili yaani viambishi vinaweza kupachikwa kabla au baada ya mzizi na huwa na uamilifu bayana.

Mfano
Hebu tuchunguze mifano ifuatayo:

Kiswahili
           Kisukuma
         Kisimbiti
              Kinyiha
A-na-lim-a
           a-le-lem-a
         a-ra-rem-a
              i-nku-lim-a
a-na-chek-a
           A-le-sek-a
          a-ra-sek-a
              a-ku-sek-a

Kwa kuangalia mifano hii utagundua kwamba katika kutenganisha viambishi hufuata kanuni moja kwamba mahali kinapokaa kiambishi kwa mfano cha njeo, ndipo pia hukaa kwa upande wa lugha za kibantu, kwa mfano –na- na –ra- katika lugha ya kisimbiti. Hivyo tunaweza kusema kuwa kuna unasaba baina ya lugha hizi

Vilevile sintaksia ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa karibu sana. Kwa mfano jinsi ya mpangilio wa vipashio na kuunda sentensi hufanana yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo hufanana katika Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili sentesi inakuwa na pande mbili yaani upande wa kiima na upande wa kiarifu, katika upande wa kiima kipashio chake kikuu ni nomino na katika upande wa kiarifu kipashio chake kikuu ni kitenzi. Hii inamaana kwamba katika kuunda sentensi ni lazima nomino ianze na baadaye kitenzi.

Mfano
Hebu tuangalie mifano ifuatayo:

Kiswahili
                       Mama / anakula                        N (K) T (A)
Kijita
                       Mai / kalya                                 N(K) T (A)
Kihehe
                       Mama/ ilya                                 N(K) T(A)
Kihaya
                       Mama / nalya                             N(K) T(A)

Katika mifano hii tumeona kwamba muunndo wa kiima-kiarifu katika lugha za kibantu unafanana sana na ule wa Kiswahili yaani nomino hukaa upande wa kiima halikadhalika kitenzi hukaa upande wa kiarifu, kwa hiyo kwa mifano hii tunaweza kusema kuwa lugha ya Kiswahili ni jamii ya lugha za kibantu.

Pia mfumo wa sauti (fonolojia) wa lugha za kibantu unafana sana na ule wa Kiswahili, yaani mpangilio wa sauti katika kuunda silabi, na miundo ya silabi kwa ujumla hufanana. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili hakuna muundo wa silabi funge yaani silabi ambayo inaishia na konsonanti, muundo asilia wa silabi za Kiswahili ni ule unaoishia na irabu vilevile katika lugha za kibantu hufuata muundo wa silabi wazi, yaani silabi zote huishia na irabu.

Mfano
Mifano ifuatayo hufafanua zaidi:
Kiswahili
             Baba
               K+I+K+I
Kikurya   
             Tata
               K+I+K+I
Kiha
             Data
               K+I+K+I
Kijita
             Rata
               K+I+K+I
Kipare
             Vava
               K+I+K+I

Tanbihi: K= konsonanti I= irabu.
Kwa mifano hii tunaona kwamba mifumo ya sauti katika lugha za kibantu hufanana na ule wa Kiswahili, kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lugha hizi ni za familia moja.

Pia vilevile mfumo wa ngeli za majina katika lugha ya Kiswahili hufanana sana na ule wa kibantu hususani katika upachikaji wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vya umoja na wingi hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa neno, hivyohivyo katika lugha za kibantu

Kwa mfano:
            Umoja
         Wingi
Kiswahili
            m-tu
         wa-tu
Kikurya
            mo-nto
         abha-nto
Kiha
            umu-ntu
         abha-ntu
Kikwaya
            mu-nu
          abha-nu

Mifano hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kwamba vipashio vyote vya umoja na wingi hujitokeza kabla ya mzizi wa neno, hivyo ni dhahiri lugha hizi zina uhusiano wa nasaba moja.

Vilevile katikaupatanisho wa kisarufilugha za kibantu na Kiswahili huelekea kufanana viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani viambishi vya nafsi.

Mfano wa viambishi vya nafsi
Kiswahili
                 Mtotoa-nalia
Kizanaki
                 Umwanaa-rarira
Kisukuma
                 Ng’wanaa-lelela
Kikurya
                 Omonaa-rakura


Tunaona hapo juu kwamba kiambishi ‘a’ cha upatanisho wa kisarufi hujitokeza katika lugha zote, hivyo tunashawishika kusema kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na kibantu.

Pamoja na ushahidi wa kiisimu kutupatia vithibitisho tosha juu ya ubantu wa Kiswahili pia kuna ushahidi mwingine kama vile ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.


Ushahidi wa Kihistoria

Ushahidi wa kihistoria huchunguza masimulizi na vitabu mbalimbali vya kale ambavyo huelezea asili na chimbuko la wakazi wa upwa wa Afrika Mashariki. Vilevile ugunduzi wa kiakiolojia huonesha kuwa kulikuwa na wakazi wa asili wa upwa wa Afrika Mashariki ambao walikuwa na utamaduni wao na maendeleo yao hata kabla ya kuja kwa wageni. Katika ushahidi wa kiethinolojia, huchunguzwa tarihi mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu wa pwani ya Afrika Mashariki na lugha yao.

Kwa ujumla vyanzo hivi vyote huonesha kuwa pwani ya Afrika mashariki ilikuwa na wakazi wake wa asili ambao walikuwa na lugha yao, utamaduni wao na pia maendeleo yao, vyanzo hivi pia huhitimisha kwa kusema kuwa lugha ya wakazi hawa ilikuwa ni Kiswahili.


Jinsi Miundo ya Kiswahili inavyofanana na Miundo ya Lugha nyingine za Kibantu

Miundo ya lugha ya za kibantu inafanana na lugha ya Kiswahili na kufanana huko hutokea katika miundo silabi ambapo zote huishia na irabu na siyo konsonanti, miundo ya sentensi, miundo ya vitenzi vya Kiswahili ni sawa na ile ya Kibantu. Kwa mfano vitenzi vya Kiswahili na kibantu vina uhusiano mkubwa hasa katika viambishi, mnyumbaliko na pamoja na mianzo na miisho ya vitenzi. Mada hii imefafanuliwa vizuri katika mada iliyotangulia hapo juu.

Waarabu na biashara ya utumwa


Kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi ya Waarabu

Katika karne ya kumi na tisa Afrika Mashariki iliingia kwenye mahusiano na mataifa mengine kama vile Marekani, Ujerumani na Uingereza. Mahusiano haya ni baada ya watu wa pwani kuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara na Waaarabu, hawa waliweka athari kubwa katika kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Wageni kutoka Ulaya walipoingia Afrika Mashariki walifanya biashara, shughuli za kidini (mishenari), elimu na utawala. Kama ilivyokuwa katika kipindi cha Waarabu, uwepo wao pia ulikuwa na athari katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na kwingineko.


Ukuaji wa Kiswahili Kimsamiati nchini Tanzania katika Enzi ya Waarabu

Waarabu hasa katika pwani ya Afrika Mashariki walifanya biashara ikiwemo biashara ya watumwa. Ilikuwepo misafara mbalimbali ya biashara kutoka pwani hadi bara. Katika misafara hiyo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasiliano hivyo Kiswahili kikaenea pia katika sehemu za bara.

Kuna mambo kadhaa waliyofanya waarabu ambayo yalichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili. Waarabu walichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:

Biashara
Waarabu walifanya biashara kati ya pwani na sehemu za bara, katika biashara yao walichangia kwa kiasi kikubwa uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kuu ya mawasiliano na ya kibiashara iliyotumiwa na wafanya biashara wa kiarabu ilikuwa ni Kiswahili, kwa hiyo kwa njia hii waliweza kueneza Kiswahili kuanzia pwani hadi maeneo ya bara kama vile Tabora, Kigoma hadi mashariki mwa Kongo.

Dini
Dini pia ni jambo ambalo liliweza kuchangia ueneaji wa lugha ya Kiswahili enzi za waarabu. Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini yao kwa undani kabisa. Kwa hivyo iliwabidi kuanzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia, lugha iliyokuwa ikitumiwa ni lugha ya Kiswahili. Na hivyo hii ikasaidia kuenea kwa lugha ya Kiswahili.

Maandishi ya kiarabu
Waarabu pia walileta hati zao zilizotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kupitia hati za kiarabu maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili yaliweza kuhifadhiwa, hivyo Kiswahili kiliweza kukua kwa vile kingeweza kuhifadhiwa katika maandishi na kusomwa wakati wowote.

Kuoana
Pia vilevile Waarabu waliofika pwani waliweza kuoana na wabantu, hii ilisababisha kizazi kipya kutokea. Na kwa sababu hiyo watoto walichukua maneno mengi kutoka kwa baba na mama yao na hivyo kuongeza msamiati katika lugha Kiswahili.



Kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi ya Wajerumani

Wajerumani waliingia katika pwani ya Afrika Mashariki katika miaka ya 1875, walifanya kila jitihada kuwatawala Waafrika ambapo katika utawala wao walifanya biashara, waliendesha shughuli za kiutawala, za kidini na kielimu. Katika shuguli zote hizo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na kukiendeleza Kiswahili. Walipongia katika pwani ya Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimekwisha enea kwa kiasi kikubwa. Kuna mambo waliyoyafanya ambayo yalisaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili kama ifuatavyo:


Kutoa mafunzo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kwa wafanyakazi wa serikali

Waliwalazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswashili, kwa sababu sheria ilikuwa ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezijiriwa katika serekali ya mjerumani. Kwa hiyo saula hili lilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wafanyakazi ambao ilikuwa ni lazima wajifuze Kiswahili ni pamona na maakida. Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za kiutawala.

Ujenzi wa shule
Shule zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika utawala wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha ya Kiswahili

Kuenea kwa utawala wa Wajerumani nchi nzima
Utawala wa wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Na kwa kuwa wafanya kazi wa serikali ya wakati huo ilikuwa ni lazima wafahamu Kiswahili, kwa hiyo kila sehemu palipokuwa na ofisi za serikali nchi nzima kulizungumzwa Kiswahili.

Shughuli za kiuchumi

Pia katika shuguli za mashamba, wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, kwa hiyo lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi ilikuwa ni Kiswahili. Kwa hiyo kutokana na sababu kwamba utawala wa kijerumani ulitoa msukumo mkubwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zao za kiutawala, hivyo suala la ueneaji wa Kiswahili lisingeepukika.


Ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi za Wajerumani

Wajerumani waliingia katika pwani ya Afrika Mashariki katika miaka ya 1875, walifanya kila jitihada kuwatawala Waafrika ambapo katika utawala wao walifanya biashara, waliendesha shughuli za kiutawala, za kidini na kielimu. Katika shuguli zote hizo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na kukiendeleza Kiswahili. Walipongia katika pwani ya Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimekwisha enea kwa kiasi kikubwa. Kuna mambo waliyoyafanya ambayo yalisaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili kama ifuatavyo:


Kutoa mafunzo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kwa wafanyakazi wa serikali

Waliwalazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswashili, kwa sababu sheria ilikuwa ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezijiriwa katika serekali ya mjerumani. Kwa hiyo saula hili lilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wafanyakazi ambao ilikuwa ni lazima wajifuze Kiswahili ni pamona na maakida.
Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za kiutawala.

Ujenzi wa shule
Shule zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika utawala wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha ya Kiswahili

Kuenea kwa utawala wa Wajerumani nchi nzima
Utawala wa wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Na kwa kuwa wafanya kazi wa serikali ya wakati huo ilikuwa ni lazima wafahamu Kiswahili, kwa hiyo kila sehemu palipokuwa na ofisi za serikali nchi nzima kulizungumzwa Kiswahili.

Shughuli za kiuchumi
Pia katika shuguli za mashamba, wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, kwa hiyo lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi ilikuwa ni Kiswahili.

Kwa hiyo kutokana na sababu kwamba utawala wa kijerumani ulitoa msukumo mkubwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zao za kiutawala, hivyo suala la ueneaji wa Kiswahili lisingeepukika.

Enzi za Wajerumani (Elimu)


Elezea ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi za Wajerumani
Wajerumani walichangia kwa sehemu kubwa kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania enzi za utawala wao. Mambo yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili enzi za utawala wa Wajerumani ni pamoja na dini, elimu, shughuli za utawala na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo.








6 comments:

  1. love it its very helful to me as a student

    ReplyDelete
  2. I like this app coz helps me so much may Allah guarantee all of you a happy life and more mafanikio

    ReplyDelete
  3. I like this !
    this how we can make sure know what is wanted.

    ReplyDelete
  4. Ts is a very cool page and all thanks to the developer it helps a lot in studies and has got a full content of Tanzanian syllabus

    ReplyDelete


EmoticonEmoticon