Write your own article idiot!
error: Content is protected !!

Wednesday, June 20, 2018

KISWAHILI: FORM THREE: Topic 1 - NGELI ZA MANENO

 Join Our Groups

TELEGRAM | WHATSAPP

Schemes of Work 2024

English Course - Free

Kenya Resources

TOPIC 1: NGELI ZA MANENO

Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi

Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.

Mfano:               
1. Maji yakimwagika hayazoleki         
2. Mayai yaliyooza yananuka sana         
3. Yai lililooza linanuka sana       
4. Maji liliomwagika halizoleki

Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.

Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.

Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:

1. Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.

2. Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.

3. Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.

4. Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.

Habari zenye Upatanishi wa Kisarufi

3 comments:

EmoticonEmoticon