Write your own article idiot!
error: Content is protected !!

Monday, June 4, 2018

KISWAHILI: FORM ONE: Topic 3 - FASIHI KWA UJUMLA

 Join Our Groups

TELEGRAM | WHATSAPP


Schemes of Work 2024


English Course - Free


Kenya Resources








TOPIC 3: FASIHI KWA UJUMLA

Fasihi ni sanaa ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake, ndoto zake, matumaini yake, migogoro yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira yake. (Wamitila, 2004). Fasili hii imejaribu kufafanua vizuri kile ambacho fasihi inajihusisha nacho, kimsingi fasihi inajihusisha na wanadamu. Vitu vya msingi tunavyoviona katika fasili hii ni kwamba fasihi ni sanaa, na fasihi inatumia lugha lakini zaidi fasihi inajihusisha na wanadamu.

Dhima za Fasihi katika Jamii

Dhima za fasihi katika jamii ni pamoja na hizi zifuatazo:

1. Kuburudisha jamii:Pamoja na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika.

2. Kuelimisha. Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa kuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi, ubaya wa ufisadi na kadhalika.

3. Kuonya jamii. Fasihi ina jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.

4. Kuunganisha jamii. Fasihi huleta watu katika jamii. Watu huunganishwa kupitia kazi mbalimbali za kifasihi, kwa mfano, kupitia nyimbo, miviga, vichekesho na kadhalika.

5. Kukuza lugha.Fasihi hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au wasomaji. Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha.

6. Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Kupitia fasihi simulizi, tamaduni na mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau na vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika.

7. Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika.

                                 
                 
                        
AINA ZA FASIHI

Kuna tanzu mbili za fasihi, ambazo ni fasihi andishi na fasihi simulizi.

1. FASIHI SIMULIZI

Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.

Sifa za Fasihi Simulizi

1. Hupitishwa kwa njia ya mdomo

2. Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika.

3. Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali

4. Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.

5. Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.

6. Aghalabu huwa na funzo fulani

Dhima za Fasihi Simulizi

1. Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira

2. Kunasihi - kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii.

3. Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao

4. Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo.

5. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii

6. Kuunganisha watu - huleta watu pamoja

7. Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.

8. Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.

9. Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.

10. Fasihi simulizi ni chombo cha mawasiliano hususani kupitia ngomezi.

Fasihi Simulizi (Maigizo) 

2. FASIHI ANDISHI

Fasihi Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno ya maandishi kupitisha ujumbe kwa hadhira.

Kuna tanzu kuu nne za Fasihi Andishi:

1. Hadithi Fupi – Hii ni kazi ya fasihi andishi yenye kisa kimoja na mhusika mkuu mmoja na maudhui yake sio changamani.

2. Riwaya –Ni kazi ya fasihi andishi yenye wahusika wengi na muundo changamani ni ndefu na maudhui yake ni mapana.

3. Tamthilia- ni kazi ya kisanaa yenye muundo wa kiugizikaji inayowasilishwa katika maandishi.

4. Mashairi - mashairi yakiwa yamechapishwa pia hutambulika kama fasihi andishi.
            
Fasihi Andishi (Riwaya)

Sifa za Fasihi Andishi
1. Hupitishwa kwa njia ya maandishi
2. Ni mali ya mtu binafsi
3. Haiwezi kubadilishwa papo kwa papo
4. Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa katika uwasilishaji wake.

Dhima za Fasihi Andishi
1. Kukuza lugha
2. Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
3. Kuburudisha
4. Kuelimisha
5. Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
6. Kuonya, kuelekeza, kunasihi

Tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

Zifuatazo ni tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi kama zilivyobainishwa katika jedwali hapa chini: 






1 comment:


EmoticonEmoticon