Kiswahili

KISWAHILI: FORM FOUR: Topic 3 – UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

TOPIC 3: UHAKIKI WA KAZI ZA
FASIHI ANDISHI
Uhakiki wa Ushairi,
Tamthiliya na Riwaya


Uhakiki
ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani
ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari
mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile,
dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k
Dhima ya Mhakiki na
Nafasi ya Mhakiki


Uhakiki
ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo
uhakiki una dhima zifuatazo:

1. Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa
urahisi;
Watunzi
wa kazi za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo
mhakiki anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi
kwa kuvifafanua kwa lugha rahisi.

2. Husaidia ukuaji wa kazi za fasihi; Mhakiki anapoonesha ubora na udhaifu
wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na kutunga
kazi iliyobora zaidi.

3. Uhakiki hukuza uelewa wa mhakiki; Kwa kuhakiki kazi mbalimbali za
fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja na mambo yanayotokea katika
jamii.

Nafasi ya Mhakiki

Mhahiki
ana nafasi kubwa katika kazi za fasihi, Mhakaki ndiye anafafanua kazi ya fasihi
ili hadhira iweze kumwelewa vizuri mtunzi wa kazi hiyo. Kwa hiyo hapa mhakiki
anasaidia kurahisisha mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi. Vilevile mtunzi huwaonyesha
watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo huwawezesha watunzi
kufanya kazi bora zaidi.


Hatua za Kufuata
wakati wa Kufanya Uhakiki


Vilevile
mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo
huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.
1.
Kwanza ni kuisoma kazi ya fasihi; hapa mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya
fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.
2.
Pili ni kuainisha na kuchambua mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hiyo
katika vipengele vya fani na maudhui.
3.
Tatu ni kutoa tathimini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.


Uhakiki wa Kazi za Fasihi Andishi

                       

UHAKIKI WA MASHAIRI
Shairi
ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato unaowasilisha
mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na hufuata utaratibu
fulani.
Mashairi
yapo ya aina mbili:
1. Mashairi huru   
2. Mashairi ya arudhi

Mashairi ya Arudhi

Haya
ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa mashairi.
Arudhi/kanuni hizi ni pamoja na:
  1. Kugawika
    kwa shairi katika beti
  2. Beti
    kuwa na idadi maalum ya mishororo.
  3. Mishororo
    ya ubeti kugawika katika vipande
  4. Mishororo
    kuwa na ulinganifu wa mizani
  5. Shairi
    kuwa na urari wa vina
  6. Shairi
    kuweza kuimbika / kuwa na mahadhi au mapigo.
  7. Kuwepo
    kwa kipokeo katika shairi
  8. Kuwa
    na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwala
  9. hairi
    kuwa na utoshelezo wa beti / kujisimamia kimaana.

Mashairi Huru

Pia
hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiozingatia lazima
ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu huweza kuwa:
  1. Lugha
    ya muhtasari
  2. Lugha
    yenye mahadhi
  3. Lugha
    ya kisanii iliyo na mafumbo na taswira
  4. Mara
    nyingine hugawika katika beti.
  5. Mishororo
    kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)
Sifa za Mashairi

Mashairi
huwa na sifa maalum zinazoyatambulisha kama kazi ya kishairi, yawe ya kimapokeo
au kimapinduzi. 
Sifa
hizi ni kama vile:
  1. Mashairi
    hutumia lugha ya mkato / muhtasari
  2. Ni
    sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundi
  3. Huwa
    na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi beti.
  4. Hutumia
    lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na jazanda.
  5. Mashairi
    huwa na sifa ya kuweza kuimbika hivyo shairi ni wimbo na wimbo ni shairi.
Dhima ya Mashairi
  1. Kupasha
    ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvuto
  2. Kuelimisha
    na kuzindua jamii.
  3. Kuendeleza
    na kukuza kipawa cha utunzi.
  4. Kuhifadhi
    msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi.
  5. Kuburudisha
    hadhira na wasomaji.
  6. Kuwasilisha
    hisia za ndani za mtu na mawazo
Hatua za Uhakiki wa
Mashairi
  1. Soma
    shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumla.
  2. Soma
    shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali na
    kuchunguza maana ya kila mojawapo
  3. Pitia
    maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu yanayotarajiwa.
  4. Soma
    shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu
    maswali.
  5. Toa
    majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririko.
Vipengele vya
Uchambuzi Wa Mashairi

1. Anwani/kichwa cha
shairi
–
Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au sentensi moja. Anwani ni kidokezo
muhimu cha kinachozungumziwa katika shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa
moja, fumbo, kinaya, kibwagizo au sehemu ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina
anwani, basi lipewe anwani inayoafikiana na maudhui au dhamira kwasentensi
isiyozidi maneno 6.


2. Maudhui – Haya ni masuala makuu au mambo
muhimu yanayohusu mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi. Kwa
mfano:
malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k. Maudhui
hung’amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa kilichomo katika shairi.

3. Dhamira / shabaha
– Ni
lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake. Dhamira ya mtunzi huwa ni
ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi
katika shairi. Mfano: Baada ya kusoma shairi, unaweza kung’amua mtunzi
alitaka kusisitiza kauli kuwa uongozi mbaya
haufai,
misitu ni uhai
n.k. Dhamira hutokana na mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa yake.

4. Mbinu na tamathali
za lugha

Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi zilizotumiwa na mshairi katika
shairi.

Mfano:                
Mazda
/ ziada / zidi – kurefusha maneno; enda
kuwa enenda
Inksari
/ muhtasari – Ni kufupisha maneno; aliyefika
kuwa alofika.  
Utohozi
– Mbinu ya kugeuza msamiati / maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika
kana kwamba ni ya Kiswahili.

Mfano:         
Time – taimu; One – Wani. Mbinu hii
vilevile huitwa ukopaji au uswahilishaji.





Taarifa Muhimu za
Mwandishi wa kila Kitabu



Mwandishi
wa fasihi ni mtu anaeweza kubuni kazi ya fasihi na kuiweka katika maandishi.
Unaposoma kazi za fasihi ni lazima ujue taarifa muhimu za mwandishi wa kazi
hiyo, ambazo ni jina, kwa sababu kila utakapokua unajibu swali ni lazima utaje
jina la mwandishi wa kitabu. Falsafa na utamaduni kujua msimamo wake, na muundo
kujua mpangilio wa matukio, mtindo kujua upekee wake na matumizi ya lugha.

2 Comments

error: Content is protected !!