Kama Hujachaguliwa Chuo Kikuu Awamu Ya Kwanza – Nini Ufanye Sasa? Je, Ujichagulie Kozi Yoyote Ile, ili mradi Uchaguliwe katika Awamu ya Pili?
Moja ya vitu ambavyo sio vya kuchezea hapa Duniani basi ni Uchaguzi wa Kozi ya kusoma Chuo Kikuu. Ni kweli umekosa kuchaguliwa lakini usikubali kufanya maamuzi ambayo yatagharimu maisha yako kwa muda mrefu. Tafadhali, usijichagulie Kozi yoyote ili mradi tu uende tu uende Chuo Kikuu.
Kama una mpango wa kuchagua mara ya pili ili kujaribu bahati yako, basi hakikisha unalenga Vyuo ambavyo havina ushindani mkali katika kuchaguliwa na wanafunzi wengi, na pia epuka Vyuo vyenye majina makubwa makubwa.
Kama kwenu uwezo unaruhusu, basi chagua Vyuo vya Private maana wanafunzi wengi huepuka hivi vyuo kutokana na gharama, hali ambayo hupelekea kupatikana nafasi.
Unaweza pia ukasoma Diploma ya hiyo Kozi kuliko kuchagua Degree yoyote na isikusaidia kitu. Zipo Diploma ambazo zina faida sana kuliko hata Degree fulani fulani.
Au kama vipi, basi subiria mwakani ujaribu tena bahati yako, lakini sio kujichagulia kozi yoyote ile.



