Je, Unaweza Kubadilisha Kozi Ukifika Chuo Kikuu? – Tazama
Kwa upande wa Vyuo vya Private huenda kusiwe na shida sana, lakini kwa upande wa Vyuo vya Serikali kazi ipo, tena sio ndogo.
Ninakuu kutoka kwenye post ya Mdau mmoja wa Jamii Forums:
“natoa angalizo hii iliwahi kunikuta na mimi ni mmoja kati ya wahanga niliochaguliwa first round mwaka 2011 nilipofika chuoni nilitaka kubadili lakini uongozi wa chuo uligoma….kuna vyuo kama Mhimbili,,UDSM,,SUA ,,udom ubadilishaji wa course ni mgumu sana maranyingi unategemea mtu ahame course moja kwenda nyingine yaani EXCHANGE…(double coincidence ) kama barter trade ..wewe unataka mihogo una karanga…kwaio tafuta mwenye mihogo ili umpe karanga…ila sijajua kwa vyuo vingine lakin kwa tahadhari hakikisha unajaza course unayoipenda hata kama huipendi jiandae kisaikolojia kuipenda vinginevyo nakushauri usubiri utajaza mwakani,,elimu haina mwisho“



