TOPIC 4: KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI UTUNGAJI WA MASHAIRI Utungaji/uandishi wa kubuni ni ule unatokana na hisia ambazo zinamsukuma mtunzi ili atunge kazi yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo vinamsumbua akilini na kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka aliwasilishe wazo lake ili hadhira ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi hukosa usingizi na hivyo hulazimika kuamka na kuandika kile kinachomsukuma akilini mwake. Mambo ya Kuzingatia katika Utungaji wa Mashairi Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja. 1. Kuona: je, mhusika…
Author: Msomi Bora
TOPIC 3: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k Dhima ya Mhakiki na Nafasi ya Mhakiki Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo: 1. Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa urahisi; Watunzi wa kazi za fasihi hutofautiana…
TOPIC 2: UENEAJI WA KISWAHILI ENZI ZA WAINGEREZA NA BAADA YA UHURU Ukuaji na Ueneaji wa Kiswahili katika enzi ya Waingereza Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Kwa kuwa nao walihitaji kutawala hawakupuuzia matumizi ya Kiswahili katika utawala wao japo hawakutumia Kiswahili kwa lengo la kukikuza lakini walijikuta wanakieneza na kukikuza bila ya wao kukusudia. Mambo waliyochangia Waingereza katika Ukuaji wa Kiswahili nchini Tanzania Waingereza walitumia Kiswahili kama nyenzo ya kusaidia shughuli zao za kiutawala. Hata hivyo kuna mambo waliyofanya waingereza yaliyosaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili, mambo…
TOPIC 1: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI Uundaji wa Maneno Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe. Njia za Uundaji Maneno Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo: Kubadili mpangilio wa herufi. Kuambatanisha maneno. Kutohoa maneno ya lugha nyingine. Uambishaji wa maneno. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura. Kuunda Msamiati kwa kubadili Mpangilio wa Herufi Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine Mfano…
TOPIC 7: KUSOMA KWA UFAHAMU KUSOMA KIMYA Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti. Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyosoma Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo: 1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatkiwa ajiluze, Je, kinachoongelewa hapa nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo. 2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo…
TOPIC 6: UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO UANDISHI WA INSHA ZA KISANAA Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira. Au, Insha ya kisanaa ni ile inayotumia lugha ya kisanaa yaani yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tashbiha, taniaba na mubalagha. Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Vilevile insha za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto na misemo kama nahau, methali na tamathali za semi.…
TOPIC 5: UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha. Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira yake. Kwa maana…
TOPIC 4: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi. Maana ya Uhakiki Uhakiki ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Hii ina maana kwamba uhakiki wa kazi za fasihi hautoki katika ombwe, kuna kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza kufanya uhakiki, na hii ndio sababu kuna nadharia kadha wa kadha za uhakiki wa…
TOPIC 3: MAENDELEO YA KISWAHILI ASILI YA KISWAHILI Neno asili ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Kutokana na fasili hii tunaona kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa. Hivyo basi asili ya lugha ya Kiswahili bado ni mjadala mrefu ambapo wataalamu mbalimbali wanahitilafiana juu ya asili au chimbuko la lugha ya kiswahili. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati na dini ya kiislamu. Wengine wanashikilia msimamo kuwa kiswahili ni kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na uchotara baadhi yao wanaoshikilia msimamo huu ni…
TOPIC 2: MJENGO WA TUNGO Maana ya Tungo Tungo ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Au tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani ambayo huweza kuwa kamili au isiyo kamili. Kwa maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda neno, neno kuunda kirai, kirai kunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu tungo huanzia neno; rejea aina za tungo. AINA ZA TUNGO Tungo neno: Tungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno ambayo ni mofimu au fonimu. Mfano; anacheza, kakimbia.…
