Close Menu
Msomi BoraMsomi Bora
    Facebook X (Twitter) Instagram Threads WhatsApp
    Msomi BoraMsomi Bora
    • HOME
    • NOTES
    • PAST PAPERS
    • BOOKS
    • OTHERS
    • KENYA
    • CONTACT US
    Msomi BoraMsomi Bora
    Home»Kiswahili»KISWAHILI: FORM THREE: Topic 6 – UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO
    Kiswahili

    KISWAHILI: FORM THREE: Topic 6 – UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO

    June 24, 20184 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp

    TOPIC 6: UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO
    UANDISHI WA INSHA ZA KISANAA
    Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini
    kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya
    tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira. Au, Insha ya kisanaa ni
    ile inayotumia lugha ya kisanaa yaani yenye tamathali za semi kama vile
    sitiari, tashbiha, taniaba na mubalagha. Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu
    nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Vilevile insha
    za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto na misemo kama nahau, methali na tamathali
    za semi.
    Muundo wa Insha
    Kwa kawaida insha inakuwa na sehemu kuu nne: kichwa cha insha, utangulizi,
    kiini na hitimisho.
    a) Kichwa cha
    insha
    ;
    Kichwa cha insha hudokeza kile
    utachokijadili katika insha yako, hubainisha wazo kuu la mada inayohusika. Kwa
    kawaida kichwa cha insha huandikwa kwa sentensi fupi. Mfano; maisha ya
    kijijini, mimba za utotoni.
    b) Utangulizi;
    Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu
    na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.
    Utangulizi unakuwa katika aya moja fupi.
    c) Kiini cha insha; Katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili
    katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi
    ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
    d) Hitimisho; Hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha
    insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichojadiliwa katika insha.
     

    JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
    JOIN US TELEGRAM CLICK HERE
    Uandishi wa Insha na Matangazo



    UANDISHI WA MATANGAZO


    Tangazo ni taarifa za wazi zinazotoa ujumbe fulani kwa walengwa wanaohusika
    na ujumbe huo. Ujumbe unaweza kuwa na lengo la kushawishi, kuarifu, kuelekeza,
    na kadhalika.
    Vipengele vya Kuzingatiwa katika Uandishi wa
    Mtangazo

    Malengo ya Matangazo
    1. Kutoa taarifa; Lengo mojawapo la matangazo ni kutoa taarifa, mfano wa matangazo yanayotoa
    taarifa ni mialiko, tangazo la kifo, alama za barabarani, matangazo ya kazi.
    2. Kuonya; Matangazo pia yana lengo la
    kuonya, kwa mfano matangazo kama vile ya kutovuta sigara, UKIMWI na kadhalika.
    3. Kushawishi; Matangazo pia yana lengo la
    kushawishi, matangazo yenye lengo hili mara nyingi ni matangazo ya biashara
    ambayo kwa kweli lengo lake ni kushawishi wateja ili wanunue bidhaa zao,
    mtangazo ya mialiko hasahasa ya tukio fulani, labda msanii anazindua albamu
    fulani na kadhalika.

    Jinsi ya Kuandika Matangazo

    Ili tangazo liweze kufanikisha kufikia lengo lililokusudiwa kuna mambo
    kadhaa ya kufanya; mambo hayo ni kama yafuatayo:
    1. Kichwa cha habari; Mara nyingi matangazo yanakuwa na kichwa cha habari, hii inasaidia
    kujua kwa haraka kuwa tangazo linahusika na kitu gani.
    2. Kuonesha aina ya bidhaa/huduma; Hiki ndicho kiini cha tangazo, hapa tangazo linaonesha ujumbe
    uliokusudiwa kufikishwa kwa wahusika, sasa ujumbe huu waweza kuwa ni bidhaa
    inayotangazwa au huduma inayotolewa au kazi inayotangazwa au mwaliko unahusu
    nini.
    3. Anwani; Hapa tangazo linaonesha
    mahali ambapo watoa tangazo walipo, yaani ofisi zao zilipo ambapo wahusika wa
    tangazo wanaweza kwenda na kuwakuta. Kama ni tangazo la mwaliko basi ni lazima
    lionesha shughuli yenyewe itafanyika wapi.
    4. Njia za mawasiliano; Kama ni tangazo la biashara au la kazi au la mwaliko ni muhimu kutoa
    mawasiliano. Mawasiliano hayo yanaweza kuwa ni namba ya simu, fax, wavuti (kwa
    taarifa zaidi), barua pepe.



    Mbinu za Uandishi wa Matangazo

    Ili tangazo liweze kuvuta umakini wa watu ni lazima liwe na mwonekanao
    fulani. Zifuatazo ni mbinu za uandishi wa matangazo.
    1. Matumizi ya picha; Matangazo mengi ya biashara huwa yanaambatana na picha, picha hizi hujaribu
    kumshawishi mteja aamini kuwa ile bidhaa ni bora na hivyo ni muhimu kuwa nayo
    au kuinunua.
    2. Maneno machache; Matangazo
    hutumia maneno machache kwa lengo la kutomchosha mlengwa lakini wakati huohuo
    maneno hayo yana nguvu ya kumshawishi mlengwa.
    3. Lugha ya kisanii; Maneno ya kisanii katika matangazo huwa ni mepesi kukumbukwa na huwa
    yanaeleweka kirahisi. Kwa mfano, matumizi ya vivumishi, litakuwa ni bonge la shoo, njoo ujinunulie pamba za ukweli, n.k. Matumizi ya mubalagha,
    kwa mfano; mtandao unaoongoza Tanzania, mganga bingwa afrika mashariki na kati
    n.k
    4. Matumizi ya watu maarufu; Matangazo mengi hususani ya biashara hupenda kutumia watu maarufu ili
    kuwashawishi walengwa. Kwa mfano kama ni tangazo juu ya bidhaa fulani, huweza
    kumwonesha pengine msanii maarufu, miss Tanzania, au mchezajia mpira maarufu.
    Sasa mlengwa anapoona kwamba hata mtu maarufu anatumia hiyo bidhaa,
    anashawishika na yeye kuitumia
                              

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp
    Previous ArticleKISWAHILI: FORM THREE: Topic 5 – UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
    Next Article KISWAHILI: FORM THREE: Topic 7 – KUSOMA KWA UFAHAMU

    Related Posts

    Uhakiki wa Tamthiliya | Form 5 and 6 | Advanced Level

    June 2, 2026

    Usaliti Mjini – Uhakiki wa Tamthiliya | Form 5 and 6

    June 2, 2026

    Shujaa Mirambo | Uhakiki wa Tamthiliya | Form 5 and 6

    June 2, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR FORM SIX – ALL TOPICS (Fasihi ya Kiswahili)

    May 6, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR FORM FIVE – ALL TOPICS (Lugha na Sarufi ya Kiswahili)

    May 6, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR ADVANCED LEVEL – Form 5 and 6

    May 6, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR FORM FOUR – ALL TOPICS

    May 6, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR FORM THREE – ALL TOPICS

    May 6, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR FORM TWO – ALL TOPICS

    May 6, 2026

    KISWAHILI NOTES FOR FORM ONE – ALL TOPICS

    May 6, 2026
    Clickable WP Image
    • Complaints
    • CONTACT US
    © 2026 Copyright. All Rights are Reserved. Msomi Bora.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.