Kiswahili

KISWAHILI: FORM FOUR: Topic 1 – KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI

JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

TOPIC 1: KUONGEZA MSAMIATI WA
KISWAHILI

Uundaji wa Maneno
Lugha
hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo
kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili
msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.
Njia za Uundaji Maneno
Uundaji
wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:
  1. Kubadili
    mpangilio wa herufi.
  2. Kuambatanisha
    maneno.
  3. Kutohoa
    maneno ya lugha nyingine.
  4. Uambishaji
    wa maneno.
  5. Kufanikisha
    sauti, umbo, mlio na sura.

Kuunda Msamiati kwa
kubadili Mpangilio wa Herufi

Neno
hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa
kwa kubadili mpangilio wa neno lingine
Mfano
  • Neno
    lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali,
    kumi,imla, mila.
  • Neno
    tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu,
    tua, viatu, tatua.




NJIA YA KUAMBATANISHA
MANENO


Kuna
njia tatu za kuambatanisha meneno
Njia ya
kurudufisha au kukariri neno
Mfano;  barabara, sawasawa, polepole, katikati,
vilevile.
Njia ya
uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti
Nomino
na Nomino
  • Punda
    + mlia unapata Pundamilia
  • Bibi
    + Shamba unapata Bibishamba
  • Afisa
    + Elimu unapata Afisaelimu
  • Mwana
    + Siasa unapata Mwanasiasa
  • Bata
    + maji unapata Batamaji


Kuunganisha kitenzi na
Nomino/Jina
  • Changa
    + moto changamoto
  • Chemsha
    + bongo chemshabongo
  • Piga
    + mbizi pigambizi
  • Zima
    + moto zimamoto


Kuunganisha maneno
mawili na kudondosha baadhi ya herufi
Mfano
  • Baraza
    la Kiswahili Tanzania BAKITA
  • Mzaliwa
    wa mahali Fulani MZAWA
  • Chama
    cha Mapinduzi CCM
  • Nyamamfu
    NYAMAFU


KUTOHOA MANENO KUTOKA
LUGHA NYINGINE
Kila
lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya
Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa kimatamshiili
ya fuate kanuniza Kiswahili.

Maneno
yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya
Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.



Mfano

Neno la Kiswahili
            Lugha ya Mwanzo
           Neno Lililotoholewa
Shule
            Kijerumani
           Schule
Salama
            Kiarabu
           Salaam
Duka
            Kihindi
           Dukan
Karoti
            Kiingereza
           Carrot
Shati
            Kiingereza
           Shirt
Picha
            Kiingereza
           Picture
Papai
            Kihispania
           Papaya
Meza
            Kireno
           Mezi
Shukrani
            Kiarabu
           Shukran
Ngeli
            Kihaya
           Engeli
Ikulu
            Kinyamwezi
           Ikulu
Ng’atuka
            Kizanaki
           Ng’atuka
Ndafu
            Kichaga
           Ndafu
Kuunda Maneno kwa Njia ya Uambishaji wa Maneno
Hii
ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa maneno
hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina husiana.
Mfano
mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama lima,
analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.
Kufananisha
sauti, sura au tabia
Mfano
  • Kengele
    – utokana na sauti ya kengele inapo pigwa
  • Pikipiki
    – hutokana na muungurumo wa pikipiki
  • Ndizi
    mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo
  • Chubwi
    – Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

Mazingira yanayoelezea
Kuhitaji Maneno Mapya

Mabadiliko
mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha-mabadiliko ya
kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia. Katika mazingira kama haya, watu
watahitaji kuwasiliana, lugha itahitaji kuunda maneno ili kuwasilisha dhana
mpya zilizoibuka. Kwa mfano, maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi, puku,
talakirishi n.k yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknoljia kwa Kiswahili.

Undaji wa Maneno
katika Miktadha mbalimbali

Mabadiliko
ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na
jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno hayo yanaweza
kuwa katika fani mbalimbali, kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni
na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo. Mfano wa msamiati ni kama vile
fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali n.k

6 Comments

error: Content is protected !!