Je, Ukisoma Shule Binafsi, Unapata Mkopo wa Kusoma Chuo Kikuu?
Jibu ni kwamba, unaweza ukapata au usipate, ila hii itategemea na mazingira kadhaa, soma hii makala hadi mwisho
Elewa kwanza Lengo la Mkopo
Mkopo hutolewa na Serikali ili kuwasaidia Wanafunzi ambao wanatoka katika Familiya zenye uwezo mdogo wa kiuchumi ili waweze kujikimu na gharama mbalimbali za kielimu au chakula wakati wakiwa Chuoni. Kwahiyo Mkopo hautolewi tu ili mradi.
Kusoma Private
Nilishuhudia mwaka fulani, Wanafunzi waliokuwa wamemaliza Form Six shule fulani hapa Dar Es Salaam wakikosa wote mkopo wa kusoma Chuo.
Ipo hivi, kama umesoma Shule ya Private ambayo Ada yake kwa mwaka ni kubwa kuliko hata ada ya Kozi ambayo unakwenda kusomea, hapa kupata mkopo ni bahati. Kwa mfano, kama ulikuwa ukilipa Milion 4 kwa mwaka, na Ada ya Kozi kwa mwaka ni Milion 2, Serikali hapa huenda ikaacha kukupa mkopo ikiamini hautashindwa kulipa hiyo Ada ya Kozi.
Kama Umesoma Private kwa Msaada, yaani kwa kusaidiwa na Mashirika au taasisi mbalimbali, basi hakikisha unaambatanisha vyeti vya vifo vya Wazazi wako, au nakala za hao waliokusaidia au kukudhamini. Hii iatasaidia pakubwa sana wewe upate mkopo kutoka Bodi ya Mikopo
Uzito wa Kozi
Kama utasoma Kozi zenye kipaumbele kwa Serikali, yaani Serikali inahitaji sana Wataalamu wa hizo Kozi, basi una nafasi kubwa ya kupata mkopo hata kama ulisoma Shule za Private. Kwahiyo, kama umesoma private basi hakikisha unachagua Kozi zenye kipaumbele kama lengo lako ni kupata mkopo.




Leave a Comment