Close Menu
Msomi BoraMsomi Bora
    Facebook X (Twitter) Instagram Threads WhatsApp
    Msomi BoraMsomi Bora
    • HOME
    • NOTES
    • PAST PAPERS
    • BOOKS
    • OTHERS
    • KENYA
    • CONTACT US
    Msomi BoraMsomi Bora
    Home»Tips»Shule za Kifahari na Zenye Ada Kubwa Tanzania
    Tips

    Shule za Kifahari na Zenye Ada Kubwa Tanzania

    August 11, 20263 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp

    Shule Ghali na Zenye Gharama Kubwa Tanzania

    JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
    JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka Future Media imetoa orodha ya shule zenye Ada ghali zaidi hii, Aidha wamesema gharama hizo hazizingatii ada peke yake bali pia michango mingine mbalimbali ambayo wazazi na walezi hupaswa kuchangia kwa viwango mbalimbali katika shule hizi. Hebu twende tukatazame Kwa kina.


    10. Morogoro International School (MIS)
    Hii inapatikana mkoani Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. MIS hutoza kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 6.4 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.


    9. International School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
    Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).


    8. Aga Khan Primary & Secondary School
    Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.


    7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
    HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.


    6:Kennedys House Schools
    Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.


    5. Saint Constantine International School
    Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.


    4. Iringa International School (ISS)
    Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.


    3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
    Ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.


    2. Braeburn International School
    Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.


    1. International School of Tanganyika (IST)
    Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.
    Hizo ni baadhi tu lakini je shuleni kwako unalipa Ada ya Kiwango Gani? Na Je Shule ulizosoma pia ulilipa Ada ya kiwango gani?

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp
    Previous ArticleForm Two Format | Necta Exams – FTNA 2026/2027 – Tanzania
    Next Article Mesp – Standard Two | Pre-Necta Exams 2026 | Download All Subjects | Series 2

    Related Posts

    Kozi zenye Kipaumbele Kikubwa cha Kupata Mkopo – Hapa Serikali Haichomoki

    July 13, 2026

    Magroup ya Mitihani na Notes Tanzania (WhatsApp Groups) – Jiunge na Pakua

    April 14, 2026

    Pakua Notes na Vitabu Vyote vya Msomi Bora

    April 13, 2026

    Badilisha Combination | Selform Tamisemi | Form Five 2025/2026 MIS

    April 13, 2026

    Tangaza Shule hapa Msomi Bora – Ni bure kabisa

    July 24, 2025

    How to Become Number One in Your Class – 9 Tips

    July 14, 2025

    How to explore talents in your students – 7 Tips

    July 14, 2025

    How to Make your Students like your Subject

    July 14, 2025

    Ways to Make your Students like You

    July 14, 2025

    Reasons Why Many Students Fail Exams

    July 14, 2025
    Clickable WP Image
    • Complaints
    • CONTACT US
    © 2026 Copyright. All Rights are Reserved. Msomi Bora.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.